Mlinda lango wa Yanga Farouq Shikalo ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda
Kenya na Uganda zitachuana wakati wa mapumziko ya kalenda ya michuano ya Kimataifa
Timu hizo hazina majukumu ya michezo ya awali kusaka nafasi ya kutinga makundi ya Afrika katika kutafuta tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Qatar mwaka 2022
Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania, Burundi na Rwanda zinakabiliwa na michezo hiyo
Tanzania itacheza na Burundi, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa huko Burundi Septemba 02 na marudiano kufanyika uwanja wa Taifa Septemba 08
Rwanda itacheza na Shelisheli
ADVERTISE HERE