Mshambuliaji kinara wa Yanga Juma Balinya amesema mchezo wa keshokutwa dhidi ya Township Rollers watapambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi
Balinya raia wa Uganda amesema wanawajibu wa kuwapa furaha mashabiki wao
"Mashabiki wetu tunawajibika kuwapa furaha, kwa niaba ya wachezaji wenzangu nawaambia tunaenda kuwapa furaha Jumamosi," amesema
"Ni mchezo wa kufa au kupona kwetu, tutahakikisha tunatimiza malengo yetu ya kusonga mbele"
Yanga iko nchini Botswana siku ya tatu leo ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo ambao umekuwa gumzo
Mabingwa hao wa kihistoria wanahitaji kushinda ugenini au kupata sare ya mabao zaidi ya moja
Mtanange huo utakuwa mbashara kupitia Azam TV Jumamosi saa kumi kamili jioni
ADVERTISE HERE