Tunao uwezo wa kushinda ugenini - Tshishimbi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Aug 2019
Tunao uwezo wa kushinda ugenini - Tshishimbi

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema wanajiandaa kikamilifu kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa Jumamosi August 24

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Tshishimbi amesema wanahitaji kufunga mabao ugenini

"Sisi tumejiandaa kupata ushindi Jumamosi, najua mchezo utakuwa mgumu lakini tutawafunga," amesema

"Hatukupanga kuruhusu bao nyumbani, Mwalimu ametuambia na sisi lazima tufunge mabao mapema ili tuweze kushinda"

"Nawaambia mashabiki wote wa Yanga watuunge mkono kwa kutuombea ili tuweze kushinda"

Kwenye mchezo huo Yanga ni lazima ifunge angalau mabao mawili ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua inayofuata

Mabingwa hao wa kihistoria wako Botswana tangu jana wakiendelea kujifua yakiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao mshindi atatinga raundi ya kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’