Muro arejea Yanga 'kiaina'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Aug 2019
Muro arejea Yanga 'kiaina'

Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amesema atajitolea kutoa hamasa kwa mashabiki ili kurudisha 'ari' ya miaka iliyopita

Muro alikuwa machachari wakati wa Uwenyekiti wa Yusufu Manji ambapo kwa kiasi kikubwa aliweza kufanya 'amsha-amsha' za nguvu na kuwafanya mashabiki wawe karibu na timu yao kila iliposhuka dimbani

Muro amejipambanua kumudu vyema kazi hiyo ya usemaji, juzi wakati Yanga ilipocheza na Polisi Tanzania mchezo wa kirafiki alipata wasaa wa kurejesha enzi zake;

"Yanga ni timu ya Wananchi, iliundwa na wafanyabishara wadogo wadogo, kiufupi wananchi wa kawaida"

"Hao Simba wanakosea kujiita timu ya Wananchi, yao ni timu ya ma Bwanyenye... Iliundwa na wageni, na ndio maana mwanzoni walijiita Sunderland"

"Hata mpaka leo wanaongozwa na ma Bwanyenye..(anawataja viongozi wa Simba) sababu asili ya timu yao ni ya ma Bwanyenye..!," ni miongoni mwa kauli zake ambazo zimezua tafrani kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki wa Yanga wakilitumia neno 'bwanyenye' kuwatania wenzao wa Simba kuwa ni ma Bwanyenye Fc

Muro ndiye aliyeasisi majina mengi ya utani ambayo mashabiki wa Yanga hutumia kuwatania wenzao wa Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’