Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten pamoja na kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa leo Ijumaa wamezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar kesho.
Ten amesema kikosi cha Yanga kiko tayari kwa mchezo huo na amebainisha kuwa Daktari wa timu amewahakikishia ni Amissi Tambwe pekee atakayekosekana katika kikosi kitakachoivaa Mtibwa Sugar kesho ukimtoa Tshishimbi.
Papi Tshishimbi atakosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Tambwe ameanza mwanzoni mwa wiki hii baada ya kukaa nje kwa zaidi ya wiki sita akisumbuliwa na majeraha ya goti.
Ten amesema Kiungo Pius Buswita atarejea kikosini baada ya swala lake la usajili kumalizwa na uongozi
Afisa Habari huyo wa Yanga amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye dimba la Taifa kuisapoti timu ili iweze kupata ushindi.
Naye kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema Yanga iko tayari kupata ushindi kwenye mchezo huo.

ADVERTISE HERE