Yanga kushusha 'mjengo' wa maana Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2019
Yanga kushusha 'mjengo' wa maana Dar

Mambo yameendelea kuwa ‘bam bam’ ndani ya Yanga kwani muda si mrefu klabu hiyo itamiliki jengo la ghorofa 14 katika Mtaa wa Mafia, jijini Dar es Salaam, litakaloiwezesha kuingiza mamilioni ya fedha.

Hayo yamefahamika jijini Arusha jana asubuhi wakati Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla alipozungumza na wanachama wao wa tawi la Kaloleni lililozinduliwa siku hiyo na wengineo kutoka maeneo mbalimbali.

Dk. Msolla aliwapongeza wanachama wa tawi hilo na wengineo wa jijini Arusha, akiahidi kuwa nao bega kwa bega katika kuijenga klabu yao.

Alisema anafurahi kuona matawi yakiendelea kuanzishwa kila kona ili kuipa mapokezi timu inapokuwa mikoani na kuisapoti klabu kwa ujumla katika mambo mbalimbali.

"Nawaomba msinunue jezi feki popote ili kufanikisha timu kuingiza pato kupitia bidhaa hiyo na endapo kuna watu wananunua, ni vyema kuwashitaki ili wachukuliwe hatua," alisema.

Dk. Msolla alisema timu yao imesajili kulingana na mahitaji ya kocha, hivyo wao kama viongozi ni jukumu lao kuhakikisha wanakuwa katika mazingira salama na wanafanya hivyo.

Baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga ni David Molinga, Patrick Sibomana, Juma Balinya, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana, Mapinduzi Balama, Ally Ally, Lamine Moro, Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Moustafa Seleman, Ally Mtoni ‘Sonso’ na wengineo.

Juu ya mikakati yao, alisema wapo mbioni kumiliki ghorofa la kisasa litakalojengwa katika eneo lao lililopo Mtaa wa Mafia, Dar es Salaam, kwa sapoti ya wafadhili mbalimbali, ikiwamo kampuni ya SportPesa.

"Tunapambana kutafuta wadhamini na tayari kuna mpango wa eneo letu la Mafia kujengwa jengo la ghorofa 14 na mwekezaji ambapo baada ya muda, hilo jengo litakuwa ni mali yetu.

"Tupo kwenye mpango wa kutafuta wadhamini, mbali na SportPesa ili kupata vyanzo vya kutuingizia fedha. Pia, tunatafuta wadhamini wengine wa kujenga kiwanja chetu cha Kigamboni," alisema Dk. Msolla.

BINGWA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’