Miongoni mwa maeneo ambayo yameimarika zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu huu, ni safu ya ulinzi
Kama ilivyotarajiwa, mkongwe Kelvin Yondani na Lamine Moro wametengeneza ukuta wa 'chuma'
Leo katika mchezo dhidi ya AFC Leopards, walinzi hao walicheza kwa maelewano mazuri
Aidha Ally Mtoni aliyehamishiwa upande wa beki ya kushoto, ameonekana kuyamudu vyema majukumu yake
Wakati walinzi hao wakifanya vizuri, nje wapo akina Ally Ally, Mustafa Suleyman, Cleofas Sospeter na Andrew Vicent!
Kwa ukuta huu wa Yanga ambao golini utalindwa na Farouk Shikalo au Metacha Mnata, haitakuwa jambo jepesi kuupenya
ADVERTISE HERE