Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hawajanufaika na ziara waliyofanya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kutokana na mazingira mabovu ya viwanja
Licha ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards leo, Zahera amesema hawakucheza vizuri kutokana na changamoto ya uwanja
"Tuna mchezo mgumu na muhimu wa marudiano dhidi ya Township Rollers, nahitaji muda kuiandaa timu lakini tunakuja kupoteza muda huku Moshi na Arusha"
"Tunacheza na Polisi kisha AFC katika viwanja vibovu hakuna jambo la maana tulilofaidika nalo hii ziara tungeweza kuifanya muda mwingine sio huu," amesema
"Jambo la msingi nina matumaini ya kwenda kufanya vema kule Botswana kwa maana tutacheza katika uwanja mzuri"
Katika mchezo wake wa kwanza mkoani Kilimanjaro Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania
Hata hivyo Yanga ilishindwa kucheza kandanda safi kutokana na hali ya uwanja
Hali hiyo pia imewakumba mkoani Arusha leo lakini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0