Mlinda lango Metacha Mnata anatarajiwa kuendelea na majukumu ya kukaa langoni kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Baada ya kukosekana kwa leseni ya Farouk Shikalo, Metacha atakuwa na jukumu la kuibeba Yanga huko Botswana kama alivyofanya jijini Dar es salaam
Metacha ni mmoja wa walinda lango bora wa Tanzania kwa sasa akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa
Uzoefu aliopata kwenye michuano ya AFCON 2019 iliyomalizika mwezi uliopita nchini Misri, umemfanya mlinda lango huyo aongeze kujiamini
Baada ya kuwa na changamoto ya makipa kwa takribani misimu miwili, msimu huu Yanga haina hofu tena katika eneo hilo kwani imesajili walinda lango wenye viwango vya Kimataifa
ADVERTISE HERE