Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo kitashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kupimana nguvu na AFC Leopards
Mchezo huo ni maalum kwa ajili ya kukiandaa kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa wiki ijayo
Huo utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga kujipima kabla ya kuelekea Botswana
Juzi Yanga ilicheza mechi ya kwanza mkoani Kilimanjaro na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania, matokeo ambayo hayakuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo
Kocha Mwinyi Zahera amesema leo atatumia kikosi chake cha kwanza
ADVERTISE HERE