Waamuzi kutoka Madagascar watachezesha mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa kati ya Township Rollers dhidi ya Yanga
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, August 24 saa tisa na nusu Alasiri nchini Botswana
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakuwa Abdoul Ohabee Kanoso akisaidiwa na Velomanana Fedinand Jinoro Jinoro na Randrianarivelo Ravonilika Harizo
Mwamuzi wa akiba ni Andofetra Avombitana Rivolala Manda Aroniaina na msimamizi ni Patrick Kangwa kutoka Zambia
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini siku ya Jumanne August 20 baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leoprads
ADVERTISE HERE