Mashabiki wa soka wilayani Moshi leo watakuwa na nafasi ya kuwashuhudia mabingwa wa kihistoria Yanga wakipepetana na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kirafiki
Kumekuwa na shamrashamra mitaani na viunga vya mji wa Moshi ambapo gumzo kubwa ni mchezo huo
Yanga imewapa heshima ya kipekee wakazi wa Moshi baada kuamua kwenda kuweka kambi mjini hapo
Kwa zaidi ya miaka 10, mkoani wa Kilimanjaro haukuwa na timu inayoshiriki ligi kuu, ujio wa Yanga umepokelewa kwa shangwe kubwa
Msimu huu Polisi Tanzania imeweka makazi yake Moshi hivyo mashabiki watapata nafasi ya kuvishuhudia vigogo vya soka nchini
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika ambapo kiingilio cha chini ni Tsh 5,000/-, Mzunguuko
Jukwaani ni Tsh 10,000/- wakati VIP ni Tsh 50,000/-