Yondani apagawisha mazoezini Moshi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Aug 2019
Yondani apagawisha mazoezini Moshi

Beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani, ameendelea kudhihirisha ubora na utemi wake ndani ya kikosi hicho na hivyo kuwaduwaza wengi, wakiwamo nyota wenzake, hasa wageni kama Patrick Sibomana, Sadney Urikhob na Lamine Moro.

Akiwa ndio kwanza amejiunga na wenzake tangu walipoanza maandalizi ya msimu, Yondani ameonekana kucharuka katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushiriki mjini Moshi, akijituma vilivyo.

Akifahamu jukumu lililopo mbele yao la mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana, amekuwa akijifua vilivyo ili kuwa fiti zaidi, huku akitengeneza upacha na Lamine.

Kama ilivyo kawaida yake, Yondani amekuwa akitumia nguvu na akili katika kuwadhibiti washambuliaji, huku pia akiendeleza utamaduni wake wa kuanzisha mashambulizi, lakini pia kupiga pasi ndefu zenye ‘macho’.

Tayari wachezaji wapya ambao hawajawahi kumuona Yondani, akiwamo Sibomana, wameanza kuvutiwa na uchezaji wake, huku Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera na wenzake wa benchi la ufundi, wakibaki wametabasamu.

Na baada ya ujio wa Yaondani, tayari kuna uhakika wa kikosi cha kwanza cha Yanga kupanguliwa, hasa katika safu ya ulinzi.

Kabla yake, beki wa kulia alikuwa akipangwa Paul Godfrey ‘Boxer’ ambapo alipoumia, nafasi yake ilichukuliwa na Ally Ally, huku kushoto akiwekwa Muharami Issa ‘Marcelo’, wakati beki ya kati kulikuwa na Lamine na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Lakini kwa sasa Yondani ‘ameipangua’ safu hiyo ambapo kwa sasa beki ya kati atasimama yeye na Lamine, wakati Mtoni akihamia kushoto kuchukua nafasi ya Marcelo ambaye anaonekana kuhitaji kuendelea kupata uzoefu hasa wa mechi za kimataifa.

Kwa upande wa beki wa kulia, kutokana na kuumia kwa Boxer, Juma Abdul huenda akaingia, lakini pia yupo Cleofas Sospeter ambaye anaweza kuimudu nafasi hiyo kutokana na uwezo wake, akiwa ameshakomaa baada ya kujifunza kutoka kwa kaka zake msimu uliopita.

Tayari Zahera ameanza kutengeneza kombinesheni hiyo ya mabeki katika mazoezi ya jana kwa kuwapanga pamoja, huku pia akiwanoa washambuliaji wake ili waweze kuwa na makali ya kufunga mabao kila wanapopata nafasi.

Kutokana na ujio wa Yondani, kikosi cha Yanga kitakachoivaa Township, kinaweza kuwa na wachezaji wa kigeni sita tu ambao ni kipa Farouk Shikalo, Lamine, Papy Tshishimbi, Juma Balinya, Sibomana na Sadney.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo wao na Township, Zahera alisema vijana wake wanaendelea kujifua akiwapa mbinu kadha wa kadha, zaidi zikiwa ni za kutengeneza nafasi za mabao na kuzitumia.

Alisema kuwa ataanza kuzifanyia kazi mbinu zao hizo leo watakapocheza na Polisi Tanzania katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika.

"Kesho (leo) tutacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki, tutaangalia jinsi gani tutacheza na Township ili tuweze kupata ushindi. Kwa upande wangu, nina matarajio makubwa ya ushindi Botswana," alisema.

Katika hatua nyingine, Zahera amesema kuwa amefarijika mno kwa ujio wa Yondani pamoja na Juma Abdul walioungana na wenzao Moshi, akiamini wataongeza kitu katika kikosi chake.

BINGWA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
32m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’