Yanga imekuwa na rekodi nzuri kila inapocheza katika uwanja wa nyumbani jijini Dar es salaam. Takwimu za msimu ya nyuma zinathibitisha hilo.
Licha ya kuanza kwa kusuasua msimu huu michezo miwili iliyocheza uwanja wa Uhuru Yanga imezoa alama nne kati ya sita. Sio matokeo mabaya.
Kesho Jumamosi inashuka tena kwenye uwanja huo kuchuana na vinara wa ligi Mtibwa Sugar.
Mtibwa Sugar imeuanza msimu huu kwa kushinda michezo yake yote mitatu iliyocheza nyumbani kabla haijalazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wake wa kwanza wa ugenini.
Yanga itashuka kwenye dimba la Taifa ikiwa haihitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi.
Kutokana na ugumu ulionekana tangu mwanzo ni dhahiri timu itakayojikusanyia alama nyingi nyumbani na kupata matokeo mazuri ugenini ndio itatwaa ubingwa.
Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa kiungo wake Papi Kabamba Tshishimbi anayetumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kufikisha kadi tatu za njano.
Benchi la Ufundi limesisitiza hawana wasiwasi juu ya kukosekana kwa kiungo huyo mahiri.
Kamusoko huenda akarudishwa chini kucheza nafasi yake kushirikiana na Raphael Daudi na Pius Buswita.
Pia Lwandamina anaweza akamtumia Said Juma Makapu ambaye msimu huu hajaweza kuonekana kwenye kikosi cha kwanza.
Amissi Tambwe aliyeanza mazoezi mwanzoni mwa wiki hii huenda akashuka dimbani ingawa hili litategemea na ripoti ya daktari juu ya utayari wake kwani amekuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja.

ADVERTISE HERE