Alichosema Mzee Akilimali kuondoka kwa Niyonzima

Admin By Admin
β€’
25 Jun 2017
Alichosema Mzee Akilimali kuondoka kwa Niyonzima
Swala la kiungo Haruna Niyonzima kuondoka Yanga limeendelea kutengeneza vichwa vya habari huku wadau mbalimbali wakitoa maoni yao baada Yanga kuamua kuachana na kiungo huyo aliyedumu Jangwani kwa miaka sita.

Jana Mzee Ibrahim Akilimali, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga alikaribishwa na EA Radio katika kipindi cha Kipenga na alitoa maoni yake kuhusu swala la Niyonzima.

Mzee Akilimali anasema hakuna wasiwasi wowote juu ya kuondoka kwa Niyonzima kwa kuwa wapo wengi walishaondoka waliokuwa wazuri Yanga akiwamo Sunday Manara na timu iliendelea kufanya vizuri.

Mzee Akilimali amesisitiza Niyonzima aondoke tu Yanga bila wasiwasi wowote kwani ana uhakika wa kupata mchezaji mwingine wa kuziba nafasi yake.

"Mwache aende tu, Yanga ni timu kubwa na walipita wachezaji wengi zaidi yake kama vile 'Computer' na wengine wengi ambao walikuwa wazuri lakini timu iliendelea kubaki na kufanya vizuri" alisema Akilimali.

Pamoja na hayo, Mzee Akilimali amesema endapo uongozi wa Yanga utaweza kusema umeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo basi wamuite yeye ili waweze kukaa chini na kuzungumza wapate muafaka mzuri katika klabu yao.

"Viongozi waliyokuwepo madarakani kwanini hawatamki kuwa sisi tumeshindwa ebu watamke basi na nina kwambia wakitamka tu leo Niyonzima atarudi" alisisitiza Mzee Akilimali.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’