Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na utamaduni wa kwenda uwanjani kuiunga mkono timu yao bila ya kusubiri kuhamasishwa na mtu
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwakalebela alisema msukumo wa shabiki kwenda uwanjani utokane na mapenzi yake kwa timu
"Shabiki unapotakiwa kuingia uwanjani ni pasheni,unapozungumzia mpira ni pasheni kuwa wewe unaupenda mpira,kwa hiyo si kwamba lazima hadi ushawishiwe Sana ndio uingie uwanjani," amesema
Kufuatia mahudhurio hafifu kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa Jumamosi iliyopita dhidi ya Township Rollers, wadau wametoa maoni tofauti ambapo wengi wameshauri kitengo cha habari klabu ya Yanga kiongezwe nguvu kwa kupatikana mtu mwenye ushawishi
Mwakalebela amesema uongozi wa klabu hiyo upo kwenye harakati za kukiboresha kitengo hicho ili kiwe na timu kubwa ya utendaji kazi kwa manufaa ya klabu