Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kikosi chao kinafanya maandalizi kabambe kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mwakalebela amesema Yanga imeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa August 23
Mwakalebela amesema wakiwa kambini, watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (August 16) na AFC Leopards (August 18)
Aidha amesema kocha Mkuu Mwinyi Zahera amewahakikishia kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers hivyo wana matumaini makubwa kuwa watapata matokeo ugenini na kufuzu raundi ya kwanza
Katika hatua nyingine Mwakalebela amesema wamefanya mawasiliano na CAF na wanatarajia kupata leseni za wachezaji wao watatu kabla ya kwenda Botswana
Amesema lengo la Yanga ni kuhakikisha wanakwenda Botswana wakiwa na kikosi chao kamili
Amasha akumbuka nyumbani
Mlinzi wa zamani wa Yanga Ahmed Amasha, leo ameukabidhi uongozi wa timu hiyo vifaa mbalimbali vya mazoezi

Amasha aliyeitumikia Yanga kati ya mwaka 1980 na 1985, amekuwa na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali kwa klabu hiyo
Amasha kwa sasa anaishi Arabuni, amewataka wadau wengine wa Yanga ambao wanaishi nje ya nchi wasiisahau timu yao