Yanga Sc mepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali iliyopelekea vifo zaidi ya 50 na majeruhi zaidi ya 60 huko mkoani Morogoro. Mioyo yetu imejeruhiwa.
Sisi Viongozi, wachezaji, wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga, tunaungana na Watanzania wote katika maombolezo haya.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi na kuwaponywa majeruhi wote huku akiwatia nguvu ndugu jamaa na marafiki walioguswa na matatizo haya.
Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un. Bwana ametoa Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe
ADVERTISE HERE