Tuweke Utaifa mbele michuano ya CAF - Manara

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
9 Aug 2019
Tuweke Utaifa mbele michuano ya CAF - Manara

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuziunga mkono Yanga, KMC na Azam Fc kwenye michuano ya CAF ili kuendelea kulinda nafasi nne zilizopatikana

Manara amewaambia mashabiki wa Simba kuwa kesho wasiende uwanja wa Taifa kuiunga mkono Township Rollers na kuizomea Yanga

Amewataka watakaoenda uwanjani waisapoti Yanga na kama hawawezi basi ni bora wakae kimya

"Imetuchukua miongo kadhaa kama nchi kupata fursa ya kuwakilishwa na vilabu vinne Kwenye Mashindano ya CAF," amesema Manara

"Ni Simba wenye mchango mkubwa sana katika hili lakini kama Taifa tunatakiwa tufanye vizuri zaidi kupitia wawakilishi wetu ili tuendelee kwa miaka ijayo kuwa na klabu nne katika mashindano ya CAF"

"Najua ni ngumu kunielewa leo , lakini nawaomba Wanasimba wote kesho msizomee Yanga, msilipe kisasi na wekeni maslahi mapana ya nchi,sisi ni waungwana na uungwana ni vitendo"

"Kama hujiwezi usiende Taifa na ikibidi kwenda na huwezi kuwashangilia bora ukae kimya"

"Najua walitukera msimu uliopita lakini tuiangalie nchi kwanza na pia tujue wao, Azam na KMC pamoja na sisi ndio tuna nafasi ya kuendelea kupewa nafasi nne tena msimu ujao"

Tafadhali watu wangu nieleweni katika hili, naiangalia Tanzania kama nchi,utani na kuzodoana kwetu utatugharimu sote,kama kuwacheka tuwacheke baadae lakini kwa sasa interest ya Tanzania iwe moja"

cut

Kwa miaka mingi, mashabiki wa Yanga na Simba hawana mazoea ya kuwa na ushirikiano (wa uwanjani) katika ngazi ya vilabu

Ni nadra sana kwa mashabiki wa Yanga kuiunga mkono Simba katika michuano ya Kimataifa ngazi ya vilabu, na hali ni hiyohiyo kwa mashabiki wa Simba kuiunga mkono Yanga

Hata hivyo kutokana na mfumo ulianzishwa na CAF wa kutoa alama kwa nchi kulingana na mafanikio ya vilabu vyake kwenye michuano ya CAF, pengine mawazo ya Manara yanaweza kuwa na manufaa sana

Kwa mara ya kwanza Tanzania imeingiza nafasi nne michuano ya CAF, baada ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita

Ndio, Simba ilichangia alama nyingi zaidi baada ya kufika robo fainali mwaka jana, lakini hata Yanga ilichangia kutokana na kufika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu

Ili kulinda nafasi zote nne, wawakilishi wote wa Tanzania wanapaswa kufanya vizuri

Kama timu zote zitatolewa mapema, basi msimu ujao Tanzania inaweza kurudi kwenye uwakilishi wa timu mbili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’