Safu ya kiungo Yanga ni hatari tupu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2019
Safu ya kiungo Yanga ni hatari tupu

Mohammed Issa 'Banka' juzi alizaliwa upya kwa kuupiga mpira mwingi dhidi ya Kariobangi Sharks wengi wakimpigia kura ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo

Akicheza sambamba na Papy Tshishimbi, Banka alitawala dimba na kuwavuruga kabisa Sharks ambao waliishia kumchezea rafu muda mwingi

Huyu ndiye Banka aliyesajiliwa na Yanga. Alihusika kidogo tu msimu uliopita baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa miezi 14

Kocha Mwinyi Zahera atakuwa na kazi kuamua nani aanze nafasi ya kiungo cha ukabaji kwani ana mafundi watupu

Banka, Tshishimbi, Feisal Salum na Abdulaziz Makame wote wana uwezo mkubwa sana kwenye nafasi hiyo

Msimu uliopita Fei Toto hakuwa na mpinzani lakini msimu huu ni dhahiri atalazimika kufanya kazi ya ziada

Hata hivyo msimu huu kocha Zahera huenda akatumia mfumo 3-4-3/3-5-2 ambao utampa uhuru wa kuwa na viungo wengi

Katika mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks, Zahera alitumia mfumo huo kwa nyakati tofauti

Aliwatumia Mustafa Suleyman, Lamine Moro na Ally Mtoni kwenye ulinzi kisha Marcelo na Balama wakiwa walinzi/viungo wa pembeni wakati Tshishimbi na Banka wakitawala dimba huku mbele kukiwa na Balinya, Sibomana na Sadney (BSS) waliokuwa washambuliaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’