Beki Paulo Godfrey 'Boxer' ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wako Zanzibar wakiendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Juzi Boxer alishiriki kuivusha Stars raundi ya kwanza michuano ya CHAN akifunga moja ya mikwaju ya penati katika ushindi wa penati 4-1 dhidi ya Kenya baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Yanga ilikuwa na nyota watano kwenye kikosi cha Stars ambao hawakushiriki mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks
Wengine ambao tayari wameripoti kambini ni mlinda lango Metacha Mnata, viungo Feisal Salum na Abdulaziz Makame
Mkongwe Kelvin Yondani anatarajiwa kutua visiwani Zanzibar kesho Alhamisi
ADVERTISE HERE