Singida United kuzindua uwanja wa Namfua mchezo dhidi ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2017
Singida United kuzindua uwanja wa Namfua mchezo dhidi ya Yanga
Mechi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC dhidi ya Singida United itakayochezwa Novemba 4 mwaka huu katika mzunguko wa tisa wa michuano ya ligi kuu ndiyo itakayozindua rasmi uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Uwanja huo ambao umefungwa kwa muda ili kupisha matengenezo, utakapofunguliwa utatumika kama dimba la nyumbani kwa timu ya Singida United ambayo kwa sasa inatumia uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma katika michuano inayoendelea ya ligi licha ya makazi yake kuwa mkoani Singida.

Akizungumza Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Singida United ,ndiye mdau mkubwa katika matengenezo hayo, amewahakikishia wapenzi wa kandanda mkoani humo kuwa uwanja huo utakuwa tayari kabla ya Novemba 4, 2017 na kuwataka wakazi wa Singida kujiandaa kuishangilia timu yao.

Kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida United imeweza kushika nafasi ya tatu kwa alama tisa ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Yanga SC ambayo imeshika nafasi ya sita kwa pointi nane.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’