Yanga imejichimbia visiwani Zanzibar kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Township Rollers
Kikosi cha Yanga chini ya kocha Mwinyi Zahera kimetua Zanzibar mapema leo na kitakuwa huko kwa siku tatu
Zahera amesema siku hizo zinatosha kabisa kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa Rollers
Ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza, Yanga inahitaji kushinda mchezo huo kwa mabao ya kutosha
Matokeo ya mchezo wa mwaka jana ni tahadhari tosha kwa vijana wa Zahera kuelekea mchezo huo
Mwaka jana Yanga ilipoteza kwa kufungwa 2-1 dhidi ya mabingwa hao wa Botswana ingawa timu waliyocheza nayo haikuwa imara kama hii ya sasa
Wachezaji wa Yanga wamehamasika sana hasa baada ya mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi juzi kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi
Wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa Jumamosi
Kocha Zahera ametaka timu yake icheze mechi mbili za kirafiki huko Zanzibar ili kuwaangalia vizuri wachezaji wake
Mcongomani huyo alijiunga na kikosi cha Yanga wiki iliyopita baada ya kumaliza mapumziko kutokana na ushiriki wake wa michuano ya fainali za Afcon akiwa na DR Congo
Mchezo wa kwanza utapigwa kesho Jumatano, saa mbili usiku dhidi ya Malindi