Yanga imewasili visiwani Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2019
Yanga imewasili visiwani Zanzibar

Mabingwa wa kihistoria Yanga wamewasili salama visiwani Zanzibar kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa Jumamosi August 10 kwenye uwanja wa Taifa

Kocha Mwinyi Zahera amesema watatumia siku tatu kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo

Akizungumza baada ya kuwasili Zanzibar, Zahera ameeleza kufurahishwa na mapokezi makubwa waliyopata visiwani humo

"Nimefurahi wametupokea vizuri sana, hii ni mara ya kwanza kwangu kufika Zanzibar," amesema

"Timu yetu iko vizuri, wenzangu walifanya kazi nzuri wakati nilipokuwa mapumziko"

"Sasa tuna siku tatu za kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa Jumamosi"

"Tutakuwa tayari kwa mchezo huo"

Kesho Jumatano Yanga inatarajiwa kucheza na Malindi Fc katika uwanja wa Amaan, kisha siku inayofuata Alhamisi kucheza na Mlandege Fc

Michezo yote itapigwa kuanzia saa mbili usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
25m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
31m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’