Uongozi Yanga wawashukuru mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2019
Uongozi Yanga wawashukuru mashabiki

NENO LA SHUKRANI

Uongozi wa klabu ya Yanga unatoa shukrani za dhati kwa Wanayanga wote, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wote kwa namna walivyoipokea wiki ya Mwananchi, na kujitokeza kwa wingi katika ushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika wiki ya Mwananchi zilizofanyika nchini kote Tanzania Bara na Visiwani.

Kama mnavyofahamu, shughuli nyingi zimefanyika kwenye wiki hii ambazo zimehusisha mambo yafuatayo;
1. Ukarabati wa Majengo ya Hospitali,Vituo vya afya,zahanati na majeno ya taasisi za umma.
2. Kutoa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji katika jamii.
3. Kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya wazi, ya umma kote nchini .
4. Kuchangia damu na kuhamasisha umma wa watanzania kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu katika Benki ya damu.

Tunaishukuru Serikali katika ngazi zote kwa kuruhusu Wanayanga kufanya mambo waliyokusudia katika wiki hii, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyoifanya wiki nzima hadi jana siku ya Kilele, Tunavishukuru Vyombo vya Habari nchi nzima kwa kazi nzuri waliyoifanya kuwahabarisha Wananchi juu ya matukio mbalimbali ya Wiki ya Mwananchi.

Tunaishukuru kamati ya Hamasa pamoja na kamati ya `utendaji ya Yanga kwa kazi kubwa ya uratibu wa shughuli hii, na zaidi tunawashukuru sana Wanayanga kwa kujitokeza kwa wingi jana kwenye hitimisho la wiki ya Mwananchi. Shukrani hizi pia ziende pamoja na pongezi za dhati za Uongozi wa Yanga kwa makundi hayo kwa kazi zao ambazo zimeipa heshima na faraja klabu yetu.

Tunafahamu sote kwamba Wiki ya Mwananchi imefikia tamati jana (juzi) kwa mafanikio makubwa sana, lakini niwakumbushe tena kwamba mbele yetu kuna jukumu lingine la mchezo wa Kimataifa dhidi ya TownShip Rollers ya Botswana siku ya `jumamosi tarehe 10.08.2019 .

Hivyo basi Tunawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, kwa ari,upendo na mshikamano ule ule wa juzi na hamasa ya Wiki nzima iendelee kwenye mchezo huo, tujitokeze kwa wingi sana kuipa nguvu timu yetu siku ya mchezo huo ili kuhakikisha tunapata ushindi.

Uongozi unaamini kwamba hamasa hii haitapoa kuelekea kwenye mchezo huo na hata Ligi itakayoanza baadaye mwezi huu.

Dr. Mshindo Msolla
Mwenyekiti-Young Africans Sports Club

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
20h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
21h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’