Jana Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks katika kuhitimisha wiki ya Mwananchi uwanja wa Taifa
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Myarwanda Patrick Sibomana akifunga bao la Yanga kwa mkwaju wa penati
Sibomana alikuwa kivutio kwa mashabiki wa Yanga walioujaza uwanja wa Taifa kutokana na umahiri wake
Kwa waliowahi kumshuhudia mkongwe Edibility Lunyamila miaka hiyo akiitumikia Yanga, basi wanaweza kukubaliana nami kuwa Sibomana anawakumbusha mkongwe huyo ambaye kwenye mchezo wa maveterani alifunga bao pekee la Yanga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Pamba
Kama ilivyokuwa kwa Lunyamila, Sibomana ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwa guu lake la kushoto, ana kasi na akili ya mpira
Kama sio umahiri wa mlinda lango wa Sharks, Sibomana angeifungia Yanga bao kwenye kipindi cha kwanza
Mchezo wa jana ulikuwa mwanzo mzuri kwake na kwa kikosi cha Yanga pia, kwani wachezaji walionyesha uwezo mkubwa