Kabla ya tukio la wiki ya Mwananchi kufanyika leo, siku chache ziizopita msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara alinukuliwa na vyombo vya habari akitamba kuwa Yanga haina ubavu wa kujaza uwanja wa Taifa
Manara alikwenda mbali zaidi kwa kusema ataacha kazi klabu ya Simba kama Yanga itajaza uwanja leo
Hata hivyo Wananchi wamedhihirisha kuwa kwao ni suala dogo sana kujaza uwanja wa Tafa unaochukua mashabiki 60,000

Kwani mpaka kufika saa sita mchana, robo tatu ya uwanja huo ilikuwa imefurika na mpaka sasa nane ulikuwa umejaa
Bila shaka wanayanga leo wamewanyamazisha wote waliokuwa wakibeza juhudi zilizokuwa zikifanyika
Uwingi wa mashabiki wa Yanga umedhihirika leo

Mgeni rasmi Waziri Dk Harisson Mwakyembe alikiri hakuwahi kushuhudia uwanja ukiwa umefurika kiasi cha leo
Wanayanga wengi hawakuwa wakijitokeza uwanjani misimu miwili iliyopita kwa kuwa hawakupata hamasa nje na ndani ya uwanja
Lakini sasa baada ya Yanga kusukwa upya, wengi wameonyesha kuwa na imani kubwa na kikosi chao
Hakuna shaka nyomi hili litakwenda mpaka mwishoni mwa msimu