Wakati Yanga ikiendelea kuzizima ndani ya jiji la Dar es salaam, baadhi ya wachezaji wake watakuwa Kenya na kikosi cha timu ya Taifa ambapo saa kumi jioni watashuka kwenye uwanja wa Moi Kasarani kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za CHAN 2020 zinazohusisha wachezaji wa ndani
Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Dar, Stars inahitaji kushinda ugenini ili iweze kusonga mbele
Aidha matokeo ya sare ya mabao pia yataisaidia Stars kusonga mbele
Katika kilele cha wiki ya Mwananchi, Yanga itawakosa wachezaji wake watano Metacha Mnata, Paulo Godfrey, Kelvin Yondani, Feisal Salum na Abdulaziz Makame ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa
Kila la kheri Stars..
ADVERTISE HERE