Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa katika siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi
Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga, Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela amesema baada ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kesho ni siku muhimu kwa Wanayanga kujumuika uwanja wa Taifa kufurahi pamoja na timu yao
"Nachukua nafasi hii kuwaambia wapenzi na mashabiki wa Yanga kuwa kesho wajitokeze kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa. Kesho tuingie kwa wingi uwanjani huku tukiendelea na shamrashara zetu," amesema
"Tunaimani washabiki wa Yanga wana kiu ya kuiona timu yao, wana kiu ya kuona umoja na mshikamano na kiu ya kuona brand ya Yanga umerudi mahali pake"
"Tumefarijika kuona mashabiki sasa wamehamasika kuipenda timu yao kama zamani hivyo tunawakaribisha mje kwa wingi uwanjani tuishangilie klabu yetu"
Mwakalebela amesema mageti ya uwanja wa Taifa yatafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi
cutKutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo michezo miwili ya utangulizi ambayo itazikutanisha timu za Bongo Fleva dhidi ya Bongo Muvi na Maveterani wa Yanga dhidi ya Maveterani wa Pamba
Baadae kutakuwa na zoezi la kukitambulisha kikosi cha Yanga kisha kufuatiwa na mchezoa wa kukata na shoka kati ya Yanga dhidi ya Kariobangi Sharks
Tiketi zimeendelea kupatikana kupitia Selcom na vituo vilivyoainishwa

