Ngasa awaita mashabiki uwanja wa Taifa Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2019
Ngasa awaita mashabiki uwanja wa Taifa Jumapili

Winga wa Yanga Mrisho Ngasa amesema kikosi cha timu hiyo kimejiandaa kuwapa burudani mashabiki keshokutwa Jumapili kwenye mchezo wa kuhitimisha wiki ya Mwananchi

Yanga itachuana na Kariobangi Sharks katika mchezo maalum wa kuhitimisha waiki ya Mwananchi, kukaribisha msimu mpya pamoja na kutambulisha kikosi cha timu hiyo na jezi

Ngasa amesema baada ya mazoezi ya wiki tatu mkoani Morogoro, sasa wameiva na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumapili wafurahi

"Siku hiyo ni ya furaha kwa mashabiki wote, tunawaomba wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa," amesema

"Tumefanya maandalizi ya kutosha, wachezaji wote tuko tayari kuwapa furaha"

Tangu kuanza maandalizi ya msimu mpya, Ngasa ni miongoni mwa wachezaji wanaon'gara kwenye kikosi cha Yanga na bila shaka atawawashia moto Kariobangi Sharks Jumapili

Kikosi cha Yanga kinaondoka leo mchana mkoani Morogoro kurejea jijini Dar es salaam ambapo msafara wa timu hiyo utapokelewa Kibaha na kusindikizwa kwa maandamano mpaka jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’