Jana Yanga ilikamilisha usajili wa mshambuliaji David Molinga kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka klabu ya FC Renaissance ambapo Yanga inaweza kumsajili moja kwa moja baada ya mkataba wake kumalizika
Molinga alitua FC Renaissance mwezi Disemba 2018 akitokea klabu ya FC Lupopo ambako alicheza pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ambaye ameuzwa Horoya AC
Wakati yeye na Makambo wakicheza FC Lupopo, Molinga ndiye aliyekuwa anaanza mara nyingi kwenye kikosi cha kwanza, Makambo akimsubiri kwenye ubao
Aidha takwimu zake za msimu uliopita zinadhirisha ukali wake katika kutikisha nyavu
Katika mechi 16 alizocheza, alipachika mabao 14 huku akifunga mabao 11 kwenye ligi kuu ya DR Congo
Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amemsifu mshambuliaji huyo akisema ni aina ya mchezaji ambaye alihitajika Yanga
Amefichua kuwa Yanga ilimtaka mshambuliaji huyo tangu mwaka jana na baada ya kumkosa ndio ikahamia kwa Makambo