Uongozi wa Yanga umeendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi Jumapili ijayo, August 04 siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi uwanja wa Taifa
Tukio hilo ambalo litatumika kutambulisha jezi na kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu wa 2019/20, litahitimishwa kwa mchezo mkali wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kariobangi Sharks
Timu maalum ya uhamasishaji inaendelea kuzunguuka mikoa Dar, Pwani na Morogoro
Leo walikuwa wakikusanya kijiji wilayani Chalinze ambapo mamia ya mashabiki walijitokeza kupata burudani

Tiketi zitaanza kupatikana kesho August 01 ambapo uongozi wa Yanga utatangaza utaratibu wa kujipatia tiketi mapema
ADVERTISE HERE