Uongozi wa klabu ya Yanga umekuwa ukiangalia uwezekano wa kulihamishia pambano la watani wa jadi jijini Mwanza na unakusudia kupeleka maombi rasmi TFF imefahamika.
Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kwenye ligi utapigwa Oktoba 28 ambapo Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo.
Moja ya sababu zinazotajwa kushawishi uongozi kutaka kuupeleka mchezo huo jijini Mwanza ni kuongeza mapato.
Uwanja wa CCM Kirumba unachukua mashabiki 35,000 waliokaa ni zaidi ya ukubwa wa uwanja wa Uhuru unaochukua mashabiki 23,000 pekee.
Pia Yanga imekuwa na rekodi nzuri inapocheza kwenye dimba hilo. Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kutumia dimba hilo kwenye mpambano wa watani wa jadi.
Hata hivyo TFF kupitia kwa Katibu Mkuu wake Wilfred Kidau imesema wanaweza kuiruhusu Yanga kufanya hivyo endapo watajiridhisha kuwa watapata fedha nyingi zaidi Mwanza kuliko wakicheza Dar es Salaam.
"Kwa upande wangu naona wakicheza hapa Dar es Salaam watapata fedha nyingi zaidi kwa kuwa bei ziko juu, eneo la tiketi za 30,000 pia ni kubwa kuliko Mwanza. Sidhani kama uwezo wa uwanja wa Kirumba na Uhuru unatofautiana sana,"Kidau amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti.
"Wao wawasilishe maombi yao Bodi ya Ligi kisha tutatazama hoja zao, tutajaribu kuwaelewesha maana ukienda Mwanza hata gharama zinakuwa kubwa kwani timu zitalazimika kusafiri na kuweka kambi kule.
"Kuna vitu vingi vinaongezeka lakini yote kwa yote tusubiri kwanza maombi yao, ni jambo linalowezekana pia."

ADVERTISE HERE