Yanga msimu huu haitanii, baada ya kumshusha mshambuliaji David Molinga 'Falcao', mmoja wa wafungaji bora wa ligi kuu ya DR Congo akipachika mabao 11 msimu uliopita akicheza klabu ya Renaissance
Alipitwa mabao matano tu na Jackson Muleka wa TP Mazembe aliyekuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 16
Umbo la mshambuliaji huyo linaweza kumfanya beki akapatwa na 'mchecheto' hata kabla ya mchezo
Ni mshambuliaji mwenye nguvu na anayefahamu kulitumia vyema umbo lake kuwapa wakati mgumu walinzi wa timu pinzani
Ujio wake unaifanya safu ya ushambuliaji ya Yanga ikamilike sasa akiungana na Juma Balinya, Sadney Urikhob na Maybin Kalengo
August 04 sio siku ya kukosa uwanja wa Taifa...!
ADVERTISE HERE