Jumapili ijayo, August 04 ndio siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi ambapo siku hiyo Yanga itacheza na Kariobangi Sharks ukiwa ni mchezo maalum wa kutambulisha kikosi pamoja na jezi za mabingwa hao wa kihistoria
Lakini kabla ya mchezo huo, kutakuwa na michezo miwili ya kirafiki, wa kwanza utawahusisha mastaa wa muziki wa kizazi kipya 'bongofleva' wakiongozwa na Ali Kiba dhidi ya mastaa wa filamu 'bongomuvi' wakiongozwa na Vicent Kigosi maarufu Ray
Mchezo wa pili utawahusishwa wakongwe waliotamba zamani kwenye klabu ya Yanga wakiongozwa na Sunday Manara 'Computer' dhidi ya wenzao wa Pamba ya Mwanza wakiongozwa na Fumo Felician
August 04 historia itaandikwa uwanja wa Taifa, hakika sio siku ya kukosa...
ADVERTISE HERE