Licha ya kuwa hatakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachoshuka dimbani kuikabili Mtibwa Jumamosi, kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ana matumaini makubwa kuwa Yanga itaibuka na ushindi.
Tshishimbi anatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi tatu za njano kwenye michezo dhidi ya Lipuli, Njombe Mji na Ndanda FC.
Aidha Tshishimbi amefurahishwa na ushirikiano mzuri kwenye kikosi cha Yanga na ndiyo sababu kubwa inayompa matumaini kuwa ushindi utapatikana hata bila yake kuwepo dimbani.
"Nafurahi kuona tunakwenda vizuri, tangu kuanza kwa ligi, hatujapoteza mchezo zaidi ya kwenda sare huu ni mwanzo mzuri.
"Kukosa mechi ya Jumamosi inaniuma ingawa siwezi kufanya chochote zaidi ya kuwahamasisha wenzangu waweze kupiga kazi," amesema Shishimbi.
Kiungo huyo amesema Yanga, ni timu kubwa na inawachezaji wengi wenye uwezo wa kuziba nafasi hiyo hivyo anaamini wenzake hawatomuangusha na watapambana kwa ajili ya kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.
Amesema kila mchezaji kwenye kikosi chao anajua umuhimu wa ushindi hivyo anaamini kila atakayepewa nafasi ya kuanza atacheza kwa nguvu na kuhakikisha wanapata ushindi.
"Nimesikia hiyo timu ndiyo inaongoza ligi inaonekana ni nzuri lakini bado ninaimani na wachezaji wenzangu hawatokubali kuona tunapoteza mchezo , " amesema.

ADVERTISE HERE