Zile kelele sijui kagoma, eti anaidai Yanga na harudi sasa zimekwisha baada ya 'Papaa' Mwinyi Zahera kurejea na kuanza majukumu ya kukinoa kikosi chake
Moja ya mambo ambao Wanayanga wanajivunia kuwa na Zahera ni ukweli na uwazi wake
Zahera alipotua Yanga timu ilikuwa na hali mbaya, lakini aliamua kubaki na uwepo wake kwa kiasi kikubwa umesaidia kupatikana kwa Yanga hii mpya
Zahera ndiye aliyeongeza 'chachu' ya michakato ya kuichangia Yanga ambapo fedha zaidi ya Bilioni moja zilipatikana
Msimu uliopita hakuwa na timu imara, lakini aliweza kutengeneza kikosi chenye ushindani
Waliokuwa wakimzushia, walitamani iwe hivyo kwani wanafahamu msimu huu 'patachimbika'
Kwa usajili uliofanyika ambapo wote yalikuwa ni mapendekezo yake mwenyewe, wapinzani wake wanajua nini kinafuata
Wapinzani wafahamu sasa, tayari yuko mkoani Morogoro, ameanza kazi!
Halafu amekuja na habari mpya, wakati wowote Yanga itampokea mshambuliaji mwingine aliyesajiliwa kuongeza nguvu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa!