Uongozi wa Yanga umesema suala la wachezaji ambao hawakuingia kambini mkoani Morogoro limeachwa kwa kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hawakufurahishwa na mgomo uliofanywa na wachezaji hao kwani walishafanya nao mazungumzo na kufikia makubaliano
"Suala la wachezaji hao nimemuachia mwalimu ndiye atakayeamua kama kuna umuhimu wa kuwatafuta na kuwarudisha tutafanya hivyo na kama hakuna basi wataendelea na mgomo wao," Dk Msolla amenukuliwa na Mwanaspoti
"Usajili uliofanywa msimu huu umezingatia kila idara hivyo mwalimu ambaye tayari kawasiri nchini atatuambia kama wanahitajika."
Dk Msolla amesema kuna wachezaji wengine wapo kambini Morogoro na wao wanamadai kama ya hao wachezaji na kuhoji hao wanauspesho gani ambao unawafanya washindwe kuwa waungwana kama wengine
Wachezaji ambao hawakuingia kambini ni Juma Abdul, Andrew Vicent na Kelvin Yondani
Hata hivyo Yondani yuko kwenye kambi ya timu ya Taifa sambamba na Metacha Mnata, Paulo Godfrey, Abdul-aziz Makame na Feisal Salum