Jana timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ilijiweka katika wakati mgumu kutinga hatua inayofuata ya michuano ya CHAN baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya timu ya Taifa ya kenya, Harambee Stars
Matokeo hayo yamewaibua wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ambaye alishangazwa na kikosi cha Stars kilichocheza jana kujaa nyota wengi wa Simba licha ya wachezaji hao kufanya mazoezi na wenzao kwa siku moja tu
Simba imeweka kambi Afrika Kusini ambapo wachezaji saba wa timu hiyo walioitwa Stars walirejea nchini kujiunga na wenzao siku mbili kabla ya mchezo
"Mchezo ulikuwa mzuri japo kwamba matokeo binafsi yangu hayajanifurahisha kwa sababu matumaini yangu hapa yalikuwa tupate ushindi. Sasa kama unakuja uwanja wa nyumbani inapatikana droo sio jambo ambalo linapendeza kwetu sisi watu wa mpira," amesema
"Kilichosababisha siwezi kukisemea sababu nadhani hiyo ni kazi ya benchi la ufundi ambalo linachambua lakini mimi kama mshabiki wa soka kitu ambacho kimenishangaza zaidi ni uwepo wa wachezaji wengi wa Simba katika timu ya leo"
"Ninachofahamu mimi kwenye mpira lazima wachezaji wawe na muunganiko. Sasa Mwalimu ni mpya, wachezaji wa Simba wamekuja jana, hawajafanya mazoezi wakaelewana na wenzao leo wanaenda kuanza wachezaji wengi namna ile sita wale, sasa najiluliza mwalimu alikuwa akitegemea nini"
cutWachezaji wa Simba walioanza mchezo huo ni Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassani Dilunga na John Bocco wakati Ibrahim Ajib aliingia kwenye kipindi cha pili
Safu ya ushambuliaji ya Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha John Bocco ilikosa makali kabisa wakishindwa kupiga hata shuti moja lililoloenga lango
Kidogo Salim Aiyee alipoingia kuchukua nafasi ya Bocco japo dakika zilikuwa zimebaki chache, aliongeza uhai kwenye safu hiyo ambayo ilimtegemea zaidi winga Iddi Selemani