Msafara wa uhamasishaji kuelekea siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi August 04 leo Jumatatu Julai 29 2019 utakuwa viwanja vya Ikulu Bagamoyo Mkabala na Nyumbani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Msafara utapokelewa na Wanachama wa Bagamoyo eneo la Mapinga saa tatu asubuhi kwa maandamano kuelekea Bagamoyo
Kulingana na ratiba iliyotolewa na uongozi wa Yanga, Jumanne Julai 30, watakuwa viwanja vya Sabasaba (Kiwanja cha Ndege) Morogoro Mjini
Mapokezi yatakuwa saa tatu asubuhi kupitia baraara ya Old Dar es Salaam hadi njia panda ya Bigwa kuelekea Kilakala na kuingia njia ya Kichangani hadi Mji Mpya kuelekea Nunge kupitia daraja la Mwere hadi round about ya Posta na Round about ya Stand ya daladala.
Msafara utaelekea Msamvu kuelekea Chamwino hadi Mafiga na kutokea Sua Road hadi round about ya Sua na kumalizia kukusanya Kijiji katika katika Kiwanja cha ndege - Sabasaba
Jumatano, Julai 31 watakuwa Chalinze Mjini Nyuma ya Polisi
Mapokezi yataanzia Mdaula saa tatu asubuhi kwa msafara hadi Chalinze viwanja vilivyopo nyuma ya Kituo cha Polisi Chalinze.
Alhamisi, August 01 watakuwa Mlandizi mjini
Msafara utapokelewa Ruvu Darajani hadi viwanja vya wazi Mlandizi.
Ijumaa, August 02 watakuwa Kibaha Maili Moja
Msafara utapokelewa Kibaha kwa Mathias kupitia Picha ya Ndege hadi Stand ya Mabasi Kibaha Maili moja (Kibaha Container)
Jumamosi, August 03 watakuwa Kigamboni Uwanja wa Swala Tuamoyo
Msafara utapoelewa Darajani Kurasini kuelekea Viwanja vya Swala Tuamoyo.
Aidha kutakuwa na utaratibu wa kuipokea timu kwa maandamano ikiwa inatokea Morogoro ambapo msafara utasindikizwa na Wanayanga wa Morogoro na kupokelewa na watu wa mkoa wa Pwani kabla ya timu kukabidhiwa kwa Wanayanga wa Dar es salaam kwa maandamamo