Hii kesi imenichafua - Manji

Mwana Jangwani By Mwana Jangwani
β€’
25 Sep 2017
Hii kesi imenichafua - Manji
Mfanyabiashara Yusuph Manji leo amewasilisha utetezi wake mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kuhusu kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Manji ametumia jumla ya dakika 215 ambazo ni zaidi ya saa tatu kujitetea.

Mbali ya Manji, pia Daktari wa Hospital ya Agha Khan, Profesa Mustapha Bapumia ameeleza kuwa Manji ana vyuma vinne kwenye moyo wake na hivyo anatembea kwenye kamba nyembamba akisema mfanyabiashara huyo ana tatizo sugu la moyo licha ya umri wake kuwa mdogo.

Aidha, amesema kwamba walipoangalia kwenye história ya matibabu yake, wamegundua amezibuliwa mishipa ya moyo wake Dubai, India na Marekani.

Katika utetezi wake Manji akiongozwa na Wakili wake, Hajra Mungula amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba anafanya kazi ya ushauri wa Kampuni za kifamilia.

Manji: Sijatendewa haki na sijasikikizwa mbele ya mahakama.

Manji: Dawa ambazo zinatajwa kwenye hati ya mashtaka, Morphiem na Benzodiazepines ni sehemu ya dawa zangu ninazotumia.

Manji: Nilitumia dawa hizo hata siku niliyohojiwa Polisi, hivyo nimechafuliwa sana katika jamii kwani hizo dawa nina uthibitisho wake.

Manji: Napenda kutoa uthibitisho wa nyaraka za maelezo ya Daktari wangu kutoka Marekani kuhusu dawa hizo.

Manji: Uthibitisho wa nyaraka hizo ulifika kwa njia ya e-mail na sekretari alitoa nakala wakati nikiwa Hospital ya muhimbili.

Manji: Historia yangu ya kiafya aya matatizo ya moyo yapo katika ukoo wetu, ambapo nilianza kusumbuliwa nikiwa na miaka 26.

Manji: Wakati nakojoa kwa ajili ya kuchukuliwa sampo ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, mlango ulikuwa wazi na nilikabidhi sampo kwa mtu aliyekuwa nyuma yangu.

Manji: Wakati sampo ya mkojo inachunguzwa sikuulizwa, wala uchunguzi haukufanyika mbele yangu.

Manji: Baada ya kutolewa sampo ya mkojo walienda kukagua nyumbani kwangu ambapo walichukua Kompyuta, Viza Card, Simu, Credit Card, Bima na saa ambapo hadi leo Polisi hawajamrudishia.

Manji: Nashangaa nakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya lakini Polisi wamechukua vitu vingine ambavyo havihusiki na hadi leo hawajanirudishia.

Manji: Hii kesi ni propaganda na inatokana na ugomvi wa kibiashara na ni mchezo mchafu, kwani hakuna asiyejua kama alikuwa anagombania Kampuni ya Tigo.

Manji: Hii kesi imenisababishia athari kubwa sana, binafsi Baba yangu alinieleza vitu 2 ambavyo ni jina zuri na maadili katika jamii.

Manji: Nimejiuzulu klabu ya Yanga kwa sababu ya dawa za kulevya na niliandika barua kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke kuachia udiwani.

Kwa hisani ya MillardAyo
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
34m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
59m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’