Kwa Raphael Daudi mbona Niyonzima atasahaulika

Admin By Admin
•
24 Jun 2017
Kwa Raphael Daudi mbona Niyonzima atasahaulika
Raphael Daudi na Kenny Ali ndio walioibeba Mbeya City kwa misimu miwili iliyopita. Yanga ilimkosa kidogo fundi Kenny Ali aliyesajiliwa na Singida United lakini imefanikiwa kumnasa Raphael Daudi na atasaini mkataba wa miaka miwili.

Raphael Daud amethibitisha kusaini mkataba wa miaka mwili wa kuicheza Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza kupitia kipindi cha Mshikemshike viwanjani cha Azam Tv, Daud alidokeza kukubaliana kwake na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

“Nimefikia makubaliano rasmi na uongozi wa timu ya Yanga kwaajili ya maandalizi ya kuichezea msimu ujao na Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani,” alisema Daudi.

Kiungo huyo alisema taratibu zote za kusaini mkataba na Yanga zimekamilika na zitasimamiwa na kaka yake atakayekuwa na wakili wake.

Daudi ambaye aliibuliwa na kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amekuwa na uwezo mkubwa wa kupachika mabao, ambapo msimu wa 2015/16 aliifungia timu hiyo ya Mbeya mabao manane Ligi Kuu na kwenye Kombe la FA.

Mabao hayo yalimfanya amzidi bao moja kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko ambaye msimu huo alifunga mabao saba katika michuano mbalimbali.

Msimu uliomalizika mwezi Mei Daudi amepachika mabao manane kwa awamu nyingine tena.

Kwa takwimu hizo zinakuonyesha ubora wa Daudi ukimlinganisha na Haruna Niyonzima.

Msimu uliomalizika Niyonzima aliifungia Yanga bao moja pekee wakati Daudi alikuwa akishindana na washambuliaji kama akina Ngoma, Mavugo, Ajib na wengine waliopachika mabao nane.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →