Yanga imeendelea kushinda michezo yake ya kirafiki baada ya leo kuwachapa mabingwa wa ligi kuu ya Burundi Agle Noir mabao 3-0
Juma Balinya na Patrick Sibomana wameendelea kun'gara kwenye kikosi cha Yanga baada ya kila mmoja kufunga tena leo
Bao la tatu la Yanga liliwekwa kambani na kiungo Mapinduzi Balama
Huo ni mchezo wa nne wa kirafiki kwa Yanga ambayo imeshinda michezo yote, ikifunga mabao 22 na kuruhusu bao moja tu
Wafungaji wa mabao ya Yanga ni Sibomana (5), Balinya (5), Ngasa (3), Balama (2), Sadney (2), Bigirimana (2), Boxer (1), Lamine (1), Tshishimbi (1)
Kesho Jumapili Yanga itashuka tena uwanja wa Jamhuri kucheza na Mawenzi Market
ADVERTISE HERE