Kwa miaka kadhaa Kamati ya Usajili na ile ya Mashindano zimekuwa zikifanya kazi pamoja, wajumbe wake wakiwa ni walewale
Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana juzi, pamoja na mambo mengine, kimezitenganisha Kamati hizo
Frank Kamugisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hizo sasa atabaki na majukumu ya Kamati ya Usajili
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema uteuzi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano utafanywa pamoja na Wajumbe wake
Uamuzi huo umefanywa ili kuipa nguvu zaidi Kamati ya Mashindano ambayo itakuwa na jukumu la kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano yote itakayoshiriki msimu unaoanza mwezi ujao
ADVERTISE HERE