Tuko tayari kuikabili Kenya - Ndayiragije

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jul 2019
Tuko tayari kuikabili Kenya - Ndayiragije

Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amesema maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya CHAN dhidi ya Kenya, yamekamilika

Keshokutwa Jumapili Julai 28, Stars itachuana na Kenya katika mchezo ambao unahusisha wachezaji wa ndani

Ndayiragije amesema baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano, amepata timu itakayoweza kuikabili Kenya Jumapili

Aidha, Ndayiragije amesema wachezaji wote wa timu hiyo wako katika hali nzuri kukiwa hakuna majeruhi

Amewataka Watanzania wote kuiunga mkono timu Jumapili ili iweze kuibuka na ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Kenya August 04

"Nawaomba Watanzania kuwa kitu kimoja kuhakikisha wanaiunga mkono timu yao ili ipate matokeo mazuri kwenye mchezo huo," amesema

"Nimepata kikosi cha wapinzani wangu nitakachopambana nacho, kuhusu kuwaangalia mechi zao mbalimbali sijafanya hivyo lakini hilo haliondoi ushindi kuelekea mchezo huo"

Amteua Bocco kuwa nahodha

Katika hatua nyingine Ndayiragije amemteua John Bocco kuwa nahodha wa timu hiyo akisaidiwa na wakongwe Juma Kaseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’