Beki mpya wa Yanga Lamine Moro ameendelea kufanya mambo makubwa mkoani Morogoro katika mazoezi ya kikosi cha timu hiyo
Ujio wa Mghana huyo na wachezaji wengine, umekiimarisha kikosi cha Yanga mara dufu
Pamoja na mabeki wengine kufanya vizuri, lakini pacha ya Lamine na Yondani ndio inayosubiriwa kwa hamu

Wawili hao bado hawajaanza kucheza pamoja kwa kuwa Yondani hakuingia kambini Morogoro kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa
Lakini hakuna shaka, wataunda safu imara ya ulinzi
Yanga imeimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuwasajili Lamine, Ally Mtoni, Ally Ally, Mwarami Issa na Mustafa Suleyman
ADVERTISE HERE