Washambuliaji Sadney Urikhob, Juma Balinya na Patrick Sibomana wametengeneza utatu wa hatari kwenye kikosi cha Yanga
Nyota hao waliotua Yanga msimu huu, wameonekana kucheza kwa maelewano zaidi wakiwa pamoja
Kutokana na aina ya uchezaji wao, kocha Noel Mwandila amekuwa akiwaweka kwenye kikosi kimoja katika mazoezi yanayoendelea mkoani Morogoro
Licha ya kuchelewa kuanza mazoezi, Sadney 'ameiva' na kwa hakika ameongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga

Juzi alipata nafasi ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya ATN Fc na kufanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 7-0
Kwenye mchezo huo, Sibomana aliondoka na mpira baada ya kufunga mabao matatu
Mpaka sasa Sibomana ameifungia Yanga mabao manne akiongoza kwa kuzifumania nyavu kwenye michezo ya kirafiki
Balinya nae amepachika mabao mawili lakini takwimu zinaonyesha ndiye mchezaji anayefanya majaribio mengi ya kufunga katika kila mchezo
cutWakati nyota hao wakifanya vizuri, mshambuliaji Maybin Kalengo nae amerejea mazoezini baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu
Kalengo alikuwa nje kwa wiki nzima baada ya kupata majeraha hayo katika mazoezi ya timu hiyo
Yanga itacheza mchezo wa kwanza wa ushindani August 04 dhidi ya Kariobangi Sharks ukiwa ni mchezo wa kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi
Mchezo huo ambao utatumika kutambulisha kikosi cha timu hiyo pamoja na jezi, utapigwa uwanja wa Taifa