K Sharks wako vizuri, kitaeleweka August 04

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2019
K Sharks wako vizuri, kitaeleweka August 04

Kariobang Sharks kutoka nchini Kenya itakuja nchini August 04 kuipima Yanga kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, utapigwa katika dimba la Taifa baada ya tukio la utambulisho wa kikosi cha Yanga

Hii itakuwa mara ya pili kwa K Sharks kuja nchini baada ya mwezi Januari mwaka huu kushiriki michuano ya Sportpesa Cup na kuibuka mabingwa

Sharks waliiondoa Yanga kwenye michuano hiyo kwa kuifunga mabao 3-2 katika mchezo ambao ulikuwa na upinzani mkali

Uongozi wa Yanga umefanya uamuzi sahihi wa kuichagua timu hiyo kwani kwa sasa ni moja ya timu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki

Mapema mwezi huu K Sharks iliisimamisha Everton ya Uingereza kwenye mchezo uliopigwa nchini Kenya na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kabla ya kushinda kwa matuta

Sharks ilipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kutwaa taji la Sportpesa

Yanga itautumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho kabla ya Kuivaa Township Rollers kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali ambao utapigwa uwanja wa Taifa kati ya August 09-11

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’