Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amevunja ukimya na kubainisha kuwa siku 15 za mapumziko alizokuwa amepewa bado hazijamalizika
Kumekuwa na sintofahamu miongoni mwa wadau wa klabu ya Yanga kutokana na kuchelewa kwa Mcongomani huyo ambapo wengine wametumia ukimya wake kuzusha habari za uongo
Zahera amesema alipewa siku 15 za mapumziko baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa nchini Misri
Amesema mapumziko hayo alianza Julai 13 hivyo bado yuko ndani ya muda
"Nitarejea Tanzania siku yoyote taarifa zinazosambazwa kuwa nimegoma sababu naidai Yanga hazina ukweli wowote," amesema
"Nilipewa mapumziko ya siku 15 kuanzia Julai 13 siku ambayo nilifika Ufaransa"
"Mimi ni kocha wa Yanga siku yoyote mtaniona, ningekuwa sirudi basi mimi mwenyewe ningesema, maisha yangu yapo hata nje ya mpira na sio kwamba mpira ndio unanipa namna ya kuishi, nina watu 42 Congo na watu wanne Ulaya, hivyo naweza kufundisha timu yoyote hata kwa miaka mitatu bila kulipwa"
Yanga imeendelea kujifua mkoani Morogoro chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila ambaye hata hivyo program zote za mazoezi anayosimamia zinaandaliwa na kocha Zahera
Β