Abdul, Dante, Yondani wajadiliwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jul 2019
Abdul, Dante, Yondani wajadiliwa Yanga

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema suala la wachezaji Kelvin Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent litajadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji

Kikao hicho kilitarajiwa kufanyika leo Jumatano, jioni

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwakalebela alisema kuwa uongozi wa timu hiyo unafahamu Wanayanga wanataka kufahamu kinachoendelea kuhusu wachezaji hao

Lakini amewataka kuwa na subira kwa kuwa miongoni mwa ajenda zitakazo jadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na suala la wachezaji hao

"Najua wengi mnataka kufahamu kuhusu hili, ni jambo muhimu lakini nawaomba muwe na subira, tutatoa taarifa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho kitakaa leo," amesema

Yondani, Abdul na Dante hawakuripoti kwenye kambi ya kikosi cha Yanga mkoani Morogoro ikielezwa wanashinikiza walipwe madai ya fedha za usajili

Yondani ameripoti kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Kenya Julai 28

Kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa Yanga umewasimamisha wachezaji hao lakini Mwakalebela hakuthibitisha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’